Not for
Reproduction
11
sw
wenyewe na wengine kutokana na majeraha mabaya.
4. Shughulikia mafuna kwa umakinifu zaidi. Mafuta yanaweza
kushika moto na mivuke hulipuka. Tumia tu kontena
zilizothibitishwa kuwekea mafuta. USIONDOE kifuniko cha
mafuta au kuongeza mafuta wakati injini inaguruma. Ongeza
mafuta tu mahali nje wakati injini umezimwa na kupoa.
Pangusa mafuta yaliyomwagika kutoka kwenye mashine.
USIVUTE sigara.
5. Fanya mazoezi ya kuendesha mashine ukiwa UMEZIMA
BAPA ili ujue udhibiti na kupata ujuzi.
6. Kagua linalofaa kukatwa nyasi na uondoe vitu vyote kama
vile vifaa vya kuchezea, waya, mawe, matawi na vitu vingine
vinavyoweza kusababisha majeraha vikirushwa na bapa au
kukatiza ukataji nyasi.
7. Weka watu na wanyama vipenzi mbali ya eneo unalokata
nyasi. ZIMA bapa, ZIMA injini, na ZIMA mashine mara moja
ikiwa mtu yeyote atakuja katika eneo hilo.
8. Kagua ngao, diflekta, swichi, udhibiti wa ubapa na vifaa
vingine vya usalama mara kwa mara uhakikishe vinafanya na
vimewekwa ipasavyo.
9. Hakikisha lebo zote za usalama zinazomeka vizuri.
Zibadilishe ikiwa zimeharibika.
10. Jikinge unapokata nyasi na uvae miwani ya usalama,
barakoa ya vumbi, suruali ndefu na viatu vyenye ukubwa
unaofaa.
11. Jua jinsi ya KUZIMA bapa na injini haraka wakati wa
dharura.
12. Kuwa mwangalifu zaidi wakati wa kupakia au kushusha kifaa
hicho kwenye trela au lori.
13. Kagua vipengee vya kinasa nyasi mara kwa mara ukitafuta
dalili za uchakaaji au uharibikaji na uvibadilishe inavyohitajika
ili uzuie majeraha kutoka kwa vitu vinavyorushwa kuingia
maeneo yasiyo na nguvu au yaliyochakaa.
Ushughulikiaji Salama wa Petroli
Ili uepuke majeraha mwilini au uhairbifu wa mali, kuwa
mwangalifu zaidi wakati wa kushughulikia petroli. Mafuta
yanaweza kushika moto haraka na mivuke hulipuka.
1. Zima sigareti zote, biri, kiko, na vyanzo vingine vya mwako.
2. Tumia tu kontena zilizothibitishwa kuwekea mafuta.
3. USIONDOE kifuniko cha mafuta au kuongeza mafuta wakati
injini inaguruma. Wacha injini ipoe kabla ya kuongeza
mafuta.
4. USIONGEZE mashine mafuta ndani ya jengo.
5. USIWEKE mashine hii au kontena ya mafuta ndani ya jengo
mahali ambapo kuna mwako wa moto wa wazi, cheche, au
taa ya kibatali kama vile kikanza maji au vifaa vingine vya
moto.
6. USIJAZE kontena za mfuta ndani ya gari au katika kitanda
cha lori au trela kwa kutumia kifaa cha plastiki cha kulazwa
kwenye gari. Weka kontena kwenye ardhi wakati wote mbali
na gari yako kabla ya kujaza mafuta.
7. Ondoa kifaa kinachoendeshwa kwa gesi kutoka kwa gari
au trela na ukiongeze mafuta kwenye ardhi. Ikiwa hii
haiwezekani, basi ongeza kifaa hicho mafuta ukitumia
kontena yenye kubebeka, badala ya nozeli ya kimiminio cha
petroli.
8. USIWASHE kifaa kinachoendeshwa kwa gesi katika gari au
trela iliyofunikwa.
9. Weka nozeli ikuwa inagusa mdomo wa tangi la mafuta au
mdomo wa kontena wakati wote hadi uongezaji mafuta
ukamilike. USITUMIE kifaa chenye nozeli ya funga-fungua
10. Ikiwa mafuta yamemwagikia nguo, badilisha nguo hizo mara
moja.
11. Kamwe usijaze tangi la mafuta kupita kiasi. Badilisha kizibo
cha mafuta na ukikaze kwa vizuri.
Uendeshaji
1. Panda na ushuke kutoka kwenye mashine ukipitia upande
wa kushoto. Kaa mbali na mianya ya kutoa wakati wote.
2. Washa injini ukiwa kwenye kiti cha mwendeshaji, ikiwa
inawezekana. Hakikisha bapa ZIMEZIMWA na breki za
kuegeza zimewekwa.
3. USIIWACHE injini ya mashine injini ikiwa inaguruma. ZIMA
injini, SIMAMISHA bapa, WEKA breki, na uondoe ufunguo
kabla ya kuondoka kutoka nafasi ya mwendeshaji kwa
sababu yoyote ile.
4. USIENDESHE mashine kama huketi ipasavyo na miguu
ikiwa kwenye vikanyagio vya miguu au pedali.
5. ZIMA BAPA na INJINI na uhakikishe bapa zimewacha
kuzunguka kabla ya kuondoa kinasa nyazi au kuzibua
mashine ya kukatia nyasi ili uzuie kukatwa vidole au mkono.
6. Lazima bapa ZIZIMWE isipokuwa wakati wa kukata nyasi.
Weka bapa zikiwa juu kabisa wakati unakata nyasi katika
eneo lisio tambarare.
7. Weka mikono na miguu mbali na bapa zinazozunguka chini
ya deki. USIWEKE mguu chini wakati BAPA ZINAZUNGUKA
au mashine inasogea.
8. USIENDESHE mashine bila kinasa nyasi chote au ngao
zote zikiwa zimewekwa vizuri na kufanya kazi. USIELEKEZE
maendeo ya kutoa upande wa watu, magari yanayopita,
madirisha au milango.
9. Punguza mwendo kabla ya kugeuka.
10. Chunga magari ukiwa karibu au ukivuka barabara.
11. ZIMA injini mara moja baada ya kukumbana na kizuizi.
Kagua mashine na utengeneze uharibifu kabla ya kuendelea
na uendeshaji.
12. Endesha mashine tu wakati wa mchana au ukiwa na taa ya
mwangaza mzuri.
13. Sogeza usukani (ikiwa ipo) POLEPOLE ili udumishe udhibiti
wakati wa mabadiliko ya kasi na mwelekeo.
14. TAHADHARI unapovuruta mizingo. Punguza kiasi cha
mizigo kwa kile unachoweza kudhibiti kwa usalama
na uunganishe mizigo kwenye bamba la kuvuta kama
ilivyoelezwa katika maelekezo ya kuunganisho.
15. Kwenye miteremko, uzito wa kifaa kinachovutwa unaweza
kusababisha kupoteza nguvu ya kukamata ardhi na kupoteza
udhibiti. Unapovuta, nenda pole pole na uwache nafasi ya
ziada kwa ajili ya kusimama.
16. USIENDESHE injini katika maeneo yaliyofunikwa. Gesi za
ekzosi ya injini huwa na monoksidi ya kaboni, sumu kali.
17. USITOE nyenzo kando ya ukuta au kizuizi. Nyezo zinaweza
kurudi nyuma upande wa mwendeshaji.
18. Tumia vifuasi vilivyoidhinishwa na mtengenezaji peke
yake. Angalia maelezo ya mtengenezaji kwa uendeshaji na
ufungaji wa vifuasi unaofaa.
Uvutaji
1. Vuta tu na mashine ambayo ina bamba lililoundwa kwa ajili
ya kuvuta. USIUNGANISHE kifaa kinachovutwa ispokuwa
katika sehemu ya kuvutia.
2. Fuata mapendekezo ya kiwandani kwa ajili ya kikomo cha
uzito kwa vifaa vilivyovutwa na kuvuta katika miteremko.
3. USIWARUHUSU watoto au watu wengine kupand kwenye
kifaa kinachovutwa.
4. Kwenye miteremko, uzito wa kifaa kinachovutwa unaweza
kusababisha kupoteza nguvu ya kukamata ardhi na kupoteza
udhibiti.
5 Nenda polepole na uwache nafasi ya ziada kwa ajili ya
kusimama.
Summary of Contents for 2691382-00
Page 3: ...N o t f o r R e p r o d u c t i o n 3 B A 4 A 5 A 6 A B 7 A 8 A B 9 A 10 A B 11 ...
Page 4: ...N o t f o r R e p r o d u c t i o n www snapper com 4 A B 12 A 13 B A 14 A B 15 A B 16 A 17 ...
Page 51: ...N o t f o r R e p r o d u c t i o n 29 es ...
Page 73: ...N o t f o r R e p r o d u c t i o n 29 fr ...
Page 95: ...N o t f o r R e p r o d u c t i o n 29 pt ...
Page 117: ...N o t f o r R e p r o d u c t i o n 29 sw ...
Page 121: ...N o t f o r R e p r o d u c t i o n 3 B A 4 A 5 A 6 A B 7 A 8 A B 9 A 10 A B 11 ...
Page 122: ...N o t f o r R e p r o d u c t i o n www snapper com 4 A B 12 A 13 B A 14 A B 15 A B 16 A 17 ...
Page 126: ...N o t f o r R e p r o d u c t i o n A B 41 C A B 42 A D C B 38 A B 39 A B 40 ...