Not for
Reproduction
www.snapper.com
12
Ukarabati
1. USIMWEKE mashine au kontena ya mafuta ndani ya jengo
ambapo mivuke inaweza kufikia mwako wazi wa moto,
cheche, au taa ya kibatali kama vile kikanza maji, tanuu,
kikausha nguo au vifaa vinigne vya gesi. Wacha injini ipoe
kabla ya kuweka mashine katika eneo lililofunikwa. Weka
kontena ya mafuta mbali na watoto katika jengo lenye
uingizaji hewa mzuri, lisilo na watu.
2. Weka injini bila nyasi, majani au grisi nyingi ili upunguze
hatari ya moto na kuchemka kwa injini.
3. Unapokamua tangi la mafuta, kamua mafuta kwenye kontena
iliyothibitishwa nje na mbali na mwale wazi wa moto.
4. Kagua breki mara kwa mara; rekebisha, karabati au badilisha
inapohitajika.
5. Weka nolti, nati na skurubu zikiwa zote zimekazwa ipasavyo
wakati wote. Hakikisha pini zote za kota ziko mahali
zinapofaa.
6. Ruhusu uingiaji wa hewa ya kutosha wakati injini inaguruma.
Gesi za ekzosi zina monoksidi ya kaboni, sumu kali isiyo na
harufu.
7. Tenganisha kebo hasi (nyeusi) kutoka kwa betri kabla
ya kufanya ukarabati au matengenezo. Kuwasha injini
kunaweza kusababisha majeraha.
8. USIITENGENEZE mashine ukiwa chini yake bila bloku za
usalama.
9. Karabati injini na ufanye mabadiliko tu wakati injini imezima.
Ondoa waya za plagi kutoka kwa plagi na uzifungilie mbali na
plagi.
10. USIBADILISHE mipangilio ya kidhibiti kasi ya injini au
kuzidisha kazi ya injini kupindukia.
11. Paka mashine grisi baada ya vipindi vilivyotajwa katika
mwongozo ili kuzuia vidhibiti kushikana.
12. Bapa za mashine ya kukatia nyasi ni kali na zinaweza
kukata. Funga bapa au vaa glavu nzito za ngozi na uwe
TAHADHARI unapozishughulikia.
13. USIPIME cheche kwa kukwaruza plagi kando ya shimo la
plagi; plagi zinaweza kuwasha gesi inayotoka kutoka kwa
injini.
14. Peleka mashine ikarabatiwe na muuzaji aliyeidhinishwa
angalau mara moja kwa mwaka na mwambie muuzaji huyo
afunge vifaa vyovyote vipya vya usalama.
15. Karabati au badilisha lebo za usalama na maelekezo
inavyohitajika.
16. Tumia tu vipuri mbadala vilivyoidhinishwa kiwandani au
vinavyolingana wakati wa kufanya ukarabati.
Summary of Contents for 2691382-00
Page 3: ...N o t f o r R e p r o d u c t i o n 3 B A 4 A 5 A 6 A B 7 A 8 A B 9 A 10 A B 11 ...
Page 4: ...N o t f o r R e p r o d u c t i o n www snapper com 4 A B 12 A 13 B A 14 A B 15 A B 16 A 17 ...
Page 51: ...N o t f o r R e p r o d u c t i o n 29 es ...
Page 73: ...N o t f o r R e p r o d u c t i o n 29 fr ...
Page 95: ...N o t f o r R e p r o d u c t i o n 29 pt ...
Page 117: ...N o t f o r R e p r o d u c t i o n 29 sw ...
Page 121: ...N o t f o r R e p r o d u c t i o n 3 B A 4 A 5 A 6 A B 7 A 8 A B 9 A 10 A B 11 ...
Page 122: ...N o t f o r R e p r o d u c t i o n www snapper com 4 A B 12 A 13 B A 14 A B 15 A B 16 A 17 ...
Page 126: ...N o t f o r R e p r o d u c t i o n A B 41 C A B 42 A D C B 38 A B 39 A B 40 ...